HAKI ZA MWANACHAMA
HAKI YA MWANACHAMA
❖Kushiriki katika shughuli zote za Chama kwa kufuata kanuni, Sheria ya vyama vya ushirika iliyopo, Kanuni, Masharti na maazimio yote ya Mikutano Mkuu
❖Kuhudhuria na kutoa maoni yake katika mikutano mkuu ya Chama.
❖Kuchagua au kuchaguliwa kuwa mjumbe / kiongozi. Kuchaguliwa kutategemea kuwa na sifa za kugombea uongozi
❖Kuweka na kutoa akiba, amana na hisa zake kwa kufuata Masharti ya Chama.
❖Kuwa mdhamini wa mikopo kwa mwanachama mwingine.
❖Kupewa taarifa ya maendeleo ya Chama kupitia Mikutano mkuu.
❖Kupewa Masharti, kutazama Mizania, Mihtasari ya mikutano Mkuu na nyaraka za Mrajis wakati wa saa za kazi.
❖Kupewa huduma ya mikopo kwa mujibu wa masharti ya Chama na Sera ya mikopo.
❖Kuomba kuitishwa kwa Mkutano Mkuu Maalum kwa mujibu wa Masharti ya Chama.
❖Kupata Gawio kama itakavyoamuliwa na Mkutano Mkuu.
❖Mwanachama ambaye uanachama wake umekoma, iwapo hadaiwi anahaki ya kurudishiwa Hisa, Akiba, Amana na haki nyingine ndani ya siku 90 kupita tangu siku uanachama ulipokoma, isipokuwa mgao wa ziada utasubiri hadi pale ukaguzi wa hesabu utakapofanyika na mizania kutolewa na wakaguzi wa nje.
❖Kuteua mrithi/warithi Kila mwanachama atamteua mrithi wake ambaye atakuwa na haki ya kulipwa hisa na mafao yote anayostahili mwanachama anapofariki kwa kufuata Sheria ya Mirathi.
❖Mwanachama ana haki ya kubadilisha jina la mrithi na kila uteuzi utaandikwa katika daftari ya wanachama na mwanachama anayehusika atatia saini yake na dole gumba.
WAJIBU WA MWANACHAMA
❖Kutii Sheria za Chama, Kanuni na Miongozo yake kama ilivyokubaliwa na Wanachama wote.
❖Kulipa ada ya kiingilio, kununua Hisa na kulipa ada zozote zitakazokuwa zimeamuliwa na Wanachama kwenye Mkutano Mkuu.
❖Kushiriki katika shughuli za kiuchumi za Chama kama zilivyoainishwa kwenye Sera za Chama.
❖Kuhudhuria Mikutano ya Chama.
❖Kuchagua Viongozi wa Chama.
❖Kutii maamuzi ya Mkutano Mkuu.
❖Kulinda na kutunza Mali za Chama.
❖Kudhamini Chama pale inapohitajika.
❖Kubeba dhamana ikiwa janga lolote litatokea. Dhamana hiyo kikomo chake ni kiasi cha Hisa alizonazo kwenye Chama.
❖Kuchagua Warithi wao.
❖Kulipa madeni aliyonayo ndani ya Chama kwa wakati uliopangwa.
❖Kulipa mkopo alioudhamini endapo mkopaji atashindwa kulipa mkopo wake bila sababu za msingi.
❖Kuwa na angalau kiwango cha chini cha Hisa kwa mujibu wa Masharti ya Chama.
❖Kuweka Akiba mara kwa mara.
❖Kutoa taarifa kwenye Uongozi wa Chama iwapo Mtumishi au Kiongozi anatoa huduma kwa upendeleo, au anatoa au kupokea rushwa.
.