AKIBA
AMANA
HISA
MIKOPO
IFAHAMU BURUTE SACCOS LIMITED..
BURUTE SACCOS LTD ni chama cha ushirika cha akiba na mikopo kwa watumishi wa umma kwa wilaya za Bukoba na Missenyi kilichosajiliwa ambacho lengo lake kuu ni kukusanya akiba kutoka kwa wanachama na kutoa mikopo kwa riba nafuu kwa wanachama.
BURUTE SACCOS LTD ilisajiliwa mnamo tarehe 11 Oktoba 2006 chini ya kifungu cha 27 cha Sheria ya vyama vya ushirika. Na 20 ya 2003 kuboresha afya ya kifedha ya watumishi wa umma kwa kuboresha huduma bora za kifedha.
Tangu kuanza kwake BURUTE SACCOS LTD imeweza kuwa na wanachama zaidi ya 1500 katika halmashauri ya wilaya ya Missenyi na Bukoba ambayo imesaidia kuinua hali yao ya kifedha kupitia akiba na mikopo yao.
AKIBA
AINA ZA AKIBA
-
1.AKIBA YA LAZIMA
Chama hupokea na kutunza akiba za wanachama kupitia makato kwenye mshahara au mwanachama anaweza kulipa kupitia benki ;kiwango cha chini cha kila mwezi ikiwa ni Tsh 40,000/= kwa kila mwanachama.Aidha chama kinalipa riba 3%-7% ya akiba za mwanachama kila mwaka .
2.AKIBA YA ELIMU
akiba hii ni akiba inayowekwa kwa ajili ya elimu .
3.AKIBA YA KUSTAAFU
Hii ni akiba inayowekwa na mwanachama kwa ajili ya manufaa ya baadae baada ya kustaafu .
HISA
Kila mwanachama anatakiwa kununua hisa 40 kwa Tsh 10,000 kwa kila hisa kukamilisha uanachama wake.
AMANA
(AMANA ILIYOWAZI)
Amana ni fedha ambayo mwanachama huweka kwa manufaa yake mwenywewe.Pia mwanachama anaweza kuweka na kuchukua mda wowote.
(AMANA ILIYOFUNGWA/YA MDA MAAALUM)
Hizi ni fedha ambazo mwanachama huweka kwa mda maalum na hawezi kuzitoa kutokana na makubaliano yaliyofikiwa baina ya chama na mwanachama.Amana maalum yaweza kuwekwa katika kipindi cha miezi mitatu(3),miezi sita(6),miezi tisa(9),miezi kumi na mbili(12).Faida katika amana maalum ni asilimia KUMI(10%)kwa mwaka
MIKOPO
MKOPO WA DHARURA
- Mkopo wa dharula hutolewa kwa kiasi kisichozidi milioni moja.
- hutolewa ndani ya miezi sita(6).
- ukiwa umetimiza vigezo vya kupata mkopo wa dharura utaupata ndani ya masaa nane PAKUA FOMU YA MKOPO WA DHARURA HAPA
MKOPO WA MAENDELEO
- Mkopo wa Maendeleo hutolewa kwa kiasi kisichozidi milioni Thelatini(30).
- hutolewa kwa miaka mitano(miezi 60). PAKUA FOMU YA MKOPO WA MAENDELEO HAPA
HUDUMA YA UWAKALA
BURUTE SACCOS LIMITED HUTOA HUDUMA YA UWAKALA NA MAKAMPUNI MBALIMBALI
BURUTE SACCOS LIMITED HUTOA HUDUMA YA UWAKALA NA MAKAMPUNI MBALIMBALI